Kampuni ya meli ya Maersk inasema kuwa inajiandaa kuruhusu meli kuanza tena safari zake kupitia bahari ya Sham, kutokana na kuanza kwa operesheni ya kimataifa ya majini inayoongozwa na Marekani ili kuzilinda meli dhidi ya mashambulizi ya waasi wa ki-Houthi nchini Yemen.
Mashambulizi ya wa-Houthi yamesababisha kuvurugika kwa safari za meli kupitia Mfereji wa Suez na Bahari ya Sham, moja ya njia muhimu zaidi kwa ajili ya biashara ya mafuta, gesi asilia, nafaka na bidhaa za reja-reja kati ya Ulaya na Asia.
Maersk alisema katika taarifa Jumapili tumepokea uthibitisho kwamba mpango wa usalama wa kitaifa uliotangazwa hapo awali Operesheni Prosperity Guardian (OPG), sasa umeanzishwa na kupelekea kuruhusu biashara ya baharini kupita katika Bahari ya Sham hadi Ghuba ya Aden na kwa mara nyingine tena kurudi na kutumia Mfereji wa Suez kama lango la kuingilia kati ya Asia na Ulaya
Forum