Iran imeanza tena kurutubisha madini ya uranium kwa kiwango kilicho sawa na mwanzoni mwa mwaka huu, IAEA imesema Jumanne wakati nchi hiyo ikiharakisha mpango wake wa nyuklia huku ikikanusha kuwa inatengeneza bomu.
Iran imeongeza uzalishaji wake wa madini ya uranium yenye utajiri mkubwa, na hivyo kupunguza uzalishaji wa awali kutoka kati-kati ya mwaka 2023, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema katika taarifa. Iran imeongeza uzalishaji wake wa madini ya uranium kwa asilimia 60 kwa kiwango cha kilo 9 kwa mwezi, tangu mwishoni mwa mwezi Novemba.
Hiyo ni kutoka kilo 3 kwa mwezi tangu Juni, na kurudi kwa kilo 9 kwa mwezi kiwango ilichokuwa ikizalisha wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka 2023, IAEA ilisema.
Tarehe 19 na 24 Desemba, wakaguzi wa IAEA walithibitisha kiwango cha uzalishaji wa madini ya uranium yaliyorutubishwa kwa kiwango hiki kwenye vituo viwili ambapo Iran inafanya shughuli hizi; Kiwanda cha Kuboresha Mafuta cha Natanz, na Kiwanda cha Kuboresha Mafuta cha Fordow, ilisema. Silaha za nyuklia zinahitaji madini ya uranium kwa asilimia 90, wakati asilimia 3.67 inatosha kwa vituo vya nyuklia.
Forum