Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 16, 2024 Local time: 20:48

Watu 5 wafariki baada ya jengo kuporomoka Kariakoo, Dar es Salaam


Jengo lililoporomoka katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania. Novemba 16, 2024.
Jengo lililoporomoka katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania. Novemba 16, 2024.

Idadi ya waliopoteza maisha yao Jumamosi kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika soko la Kariakoo mjini Dar es Salaam, Tanzania, imeongezeka na kufikia watu watano, kwa mujibu wa mamlaka.

Kamanda wa uokoaji kutoka jeshi la Zima moto nchini Tanzaia Peter Mtui, amesema wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa huku 46 wakiokolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo, Mtui amesema kazi ya uokoaji inaendelea kwa kushirikiana na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikiongozwa na na jeshi la Zima moto, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JKT), Jeshi la Polisi na wanamgambo.

Awali Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa alikuwa maesema ni mtu mmoja tu aliyefariki, na kuagiza timu nzima ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kupeleka mitungi ya Oxygen eneo la tukio ili kuokoa maisha ya manusura walioporomokewa na jengo hilo.

Majaliwa alisema waokoaji wangetumia kila mbinu kuhakikisha waliokwama huko chini wanaokolewa kwa njia salama.

‘’Nataka niwahakikishie kwamba, kazi hii tutaendelea nao, niwahakikishe kwamba kazi hii tutaaendelea nayo, kuhakikisha kuwa kuokoa hadi mtu wa mwisho,’’ amesema Majaliwa.

"Uzuri tumeambiwa ndugu wanaendelea kupata mawasilianao na ndugu zao waliopo hapo chini na uzuri nimeona nikiwa hapa mmoja aliyeokolewa amesema wenzangu wapo chini, kwa hiyo kazi inaendelea ya kuwaokoa waliopo chini na nataka tuhakikishe hapa hatutumii nguvu tutatumia akili zaidi," amesema Majaliwa.

Majaliwa alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kutokana na ajali hiyo, huku akiagiza nguvu ya uokoaji iongezwe ili kunusuru maisha ya waathirika wa ajali hiyo.
Jengo hilo la ghorofa nne limeanguka leo Jumamosi Novemba 16, 2024 majira ya saa tatu asubuhi.

- Egberth Alfred amechangia ripoti hii

Forum

XS
SM
MD
LG