Waliohudhuria, ambao walikusanyika karibu na makao makuu ya shirika la habari la BBC , walianza kutembea katika barabara za mji huo kabla ya mkutano wa alasiri, karibu na bunge na afisi na makazi ya Waziri Mkuu Rishi Sunak ya Downing Street.
Baadhi yao walipeperusha bendera na mabango ya Palestina -- yenye jumbe kama "uhuru kwa Palestina", "komesha mauaji" na "vikwazo kwa Israel" -- walipokuwa wakielekea eneo ambapo hotuba zilipangwa kutolewa.
"Nadhani watu wote tu duniani kote, siyo tu nchini Uingereza, lazima wasimame na kutoa wito wa kukomeshwa kwa wazimu huu," Ismail Patel, mwenyekiti wa kampeni ya Friends of Al-Aqsa, aliliambia shirika la habari la AFP wakati wa maandamano hayo.
"Vinginevyo, katika siku chache zijazo, huenda tukashudia janga likitokea."
Maandamano hayo yanakuja wakati Israeli inazidisha vita vyake kuharibu uwezo wa Hamas, ikishambualia mara kwa mara Ukanda wa Gaza na kupeleka maelfu ya wanajeshi karibu na mpaka wake na Gaza kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa katika eneo hilo.
Hayo yanafuatia shambulio la Jumamosi iliyopita la Hamas, ambapo mamia ya wapiganaji wa kundi hilo la wanamgambo walivuka mpaka wa Israel na kuchukua mateka na kuua zaidi ya raia 1,000 mitaani, majumbani mwao au kwenye tafrija ya muziki.
Forum