Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 17:16

Jeshi la israel limewataka raia wa Gaza City kuhamia Kusini


Wa-Palestina wakifukua vifusi vya majengo yaliyoshambuliwa na ndege za Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Al Shati, Oct. 12, 2023.
Wa-Palestina wakifukua vifusi vya majengo yaliyoshambuliwa na ndege za Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Al Shati, Oct. 12, 2023.

Jeshi la Israel siku ya Ijumaa limetoa wito kwa raia wote huko Gaza City ambayo ina idadi ya zaidi ya watu milioni moja kuhamia kusini ndani ya saa 24 wakati ikikusanya vifaru kabla ya uvamizi wa ardhini uliotarajiwa baada ya shambulio baya kufanywa na kundi la wanamgambo wa Hamas.

"Huu ni wakati wa vita," Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema Alhamis wakati ndege za kivita za Israel zikiendelea kuishambulia Gaza ikilipiza kisasi mashambulizi ya wikiendi yaliyofanywa na wanamgambo wa Hamas ambayo yaliua zaidi ya wa-Israel 1,300 wengi wao raia.

Jeshi la Israel lilisema litafanya kazi kwa kiasi kikubwa huko Gaza City kwa siku kadhaa zijazo na kwamba raia wanapaswa kurudi pale wanaposhauriwa. Zaidi ya wa-palestina 1,500 tayari wameshauawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.

"Raia wa Gaza City ondokeni muende eneo la kusini kwa usalama wako na kwa usalama wa familia yako, jiweke kando, wewe mwenyewe na magaidi wa Hamas ambao wanawatumia nyinyi kama ngao yao", jeshi lilisema.

"Magaidi wa Hamas wanajificha Gaza City ndani ya mifereji ya chini ya ardhi na ndani ya majengo yaliyojaa watu wa gaza wasio na hatia".

Ofisa mmoja wa hamas aliwasihi watu kutofuata kile alichokiita "Propaganda za uongo". Kitengo chao cha jeshi baadae kilisema kwamba miongoni mwa watu 13 waliokamatwa kutoka Israel waliuawa katika mashambulizi ya anga ya hivi karibuni ya Israel.

Mjumbe wa Palestina nchini Japan aliwashutumu wa-Israel kwa kutaka kuiangamiza Gaza wakati Umoja wa Mataifa ukisema kuwa inafikiria kwamba haiwezekani kwa harakati kama hizo za watu kufanyika "bila madhara makubwa ya kibinadamu".

Forum

XS
SM
MD
LG