Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:54

Waziri wa Ulinzi wa Marekani anasema Pentagon iko tayari kuisaidia Israel

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya NATO mjini Brussels. October 11, 2023.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya NATO mjini Brussels. October 11, 2023.

Austin alisema silaha za kijeshi, uwezo wa ulinzi wa anga pamoja na vifaa na rasilimali nyingine zilikuwa zinatolewa haraka na Washinton kwenda kwa mshirika wa karibu wa Mashariki ya Kati. 

Waziri wa Ulinzi wa Marekani LIoyd Austin alisema Ijumaa kwamba Pentagon ilikuwa tayari kupeleka misaada zaidi ya kijeshi kwa Israel wakati vikosi vya Israel vikijiandaa kwa uwezekano wa kuivamia Gaza katika kujibu shambulizi baya lililofanywa na kundi la wanamgambo wa Hamas.

Austin alisema silaha za kijeshi, uwezo wa ulinzi wa anga pamoja na vifaa na rasilimali nyingine zilikuwa zinatolewa haraka na Washinton kwenda kwa mshirika wa karibu wa Mashariki ya Kati.

Israel imeapa kuliangamiza kundi la Hamas, kundi la ki-Islam la Palestina ambalo linatawala Gaza.

Israel ilifanya mashambulizi makali sana kuwahi kutokea huko Ukanda wa Gaza baada ya Hamas kufanya shambulizi la mpakani ambalo halijawahi kutokea na la kushtukiza kusini mwa Israel hapo Oktoba 7.

Majibu ya Israel ambayo tayari yamehusisha kuangusha maelfu ya mabomu huko Ukanda wa Gaza yanatarajiwa kuongezeka wakati ikijiandaa na uwezekano wa mashambulizi ya ardhini katika ukanda mwembamba wa pwani ambao una watu wengi zaidi.

Marekani na washirika wengine wa mataifa ya magharibi wamesema wataiunga mkono Israel wakati ikifanya kile viongozi wa Israel wanasema itakuwa vita vya muda mrefu.

Forum

XS
SM
MD
LG