Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 13:45

Marekani: Bado haijajulikana iwapo Scalise atakuwa spika wa Baraza la Wawakilishi


Steve Scalise
Steve Scalise

Warepublican katika Baraza la Wawakilishi walipiga kura 113 dhidi ya 99 jana Jumatano kumteua Steve Scalise ili kuhudumu kama spika.

Lakini wingi wao mdogo katika Bunge na migawanyiko ndani ya chama chao kunaacha hali ya kutokuwa na uhakika iwapo Scalise atapanda na kushika wadhifa huo wa uongozi. .

Mconservative Mrepublican, Matt Gaetz, ambaye alilazimisha hatua ya kihistoria ya kumuondoa Spika Kevin McCarty wiki iliyopita, hivi sasa anapongeza uchaguzi mpya wa Warepublican wa mtu wa kuliongoza Baraza la Wawakilishi.

Matt Gaetz
Matt Gaetz

Katika kikao cha faragha jana Jumatano, Warepublican katika Baraza la Wawakilsihi walipiga kura kumteua Mrepublican Steven Scalise dhidi ya mconservative Mrepublican Jim Jordan katika Bunge.

Mbunge Steve Scalise, Mrepublican amesema:“Tunaona jinsi ilivyo hatari sana duniani, na jinsi mambo yanavyoweza kubadilika haraka. Tunahitaji kuhakikisha kuwa tunapeleka ujumbe kwa watu kote duniani kwamba Bunge liko wazi na watu wanfanya kazi kama kawaida.”

Mpaka spika mpya atakapochaguliwa, Bunge la Marekani halitaweza kupitisha sheria, ikiwemo msaada muhimu kwa Israel na Ukraine.

Mbunge Michael McCaul, Mwenyekiti Kamati ya Mambo ya Nje katika Bunge anaeleza:“Taifa haliwezi kumudu hali hii. Watu wa Marekani hawawezi kumudu hili. Tunahitaji spika katika kiti. Tuko katika nyakati hatari sana hivi sasa. Tuko katika mizozo mitatu mikubwa ulimwenguni, na hatuwezi kumudu kutokuwa na spika kwenye kiti.”

Michael McCaul
Michael McCaul

Lakini upigaji kura kamili umecheleweshwa hadi leo Alhamisi wakati Scalise akifanya kazi ya kuweza kupata kura 217 zinazohitajika katika kuchaguliwa, anaweza kumudu kupoteza kura nne tu za Warepublican wakati akifikiria kuwa Wademocrat wote watakuwa dhidi yake, ambapo ndivyo ilivyo. Walau Warepublicam wachache katika Bunge wanasema hawatampigia kura Scalise.

Spika wa zamani McCarthy amewaambia Warepublican mapema wiki hii wasimteue tena.

Kevin McCarthy
Kevin McCarthy

Mbunge Kevin McCarthy, Mrepublican amesema:“Nafahamu wengi wenu mnataka kuniteua – nimewaambia tafadhali msinitue.”

Scalise yuko mbele kuwania nafasi ambayo ni ya pili katika kushika wadhifa wa urais. Alijeruhiwa vibaya sana na mtu aliyekuwa na silaha wakati alipofyatua risasi kwa wabunge ambao walikuwa katika mchezo wa baseball mwaka 2017. Alipata afueni na kuendelea kuhudumu katika uongozi wa Baraza la Wawakilishi, hata baada ya kutangaza mapema mwaka huu kuwa wamegundulika kuwa ana saratani ya damu.

Ripoti ya Mwandishi wa VOA Katherin Gypson.

Forum

XS
SM
MD
LG