Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:35

Watu 34 wakiwemo watoto watano wajeruhiwa Kyiv, hakuna taarifa za vifo


Waokoaji wakifukua kufusi cha jumba lililoharibiwa huko Uman, Cherkasy Oblast, iliyoko katikati ya Ukraine, Aprili 28, 2023, baada ya makombora ya Russia kupiga miji kadhaa ya Ukraine usiku kucha.
Waokoaji wakifukua kufusi cha jumba lililoharibiwa huko Uman, Cherkasy Oblast, iliyoko katikati ya Ukraine, Aprili 28, 2023, baada ya makombora ya Russia kupiga miji kadhaa ya Ukraine usiku kucha.

Russia imefanya mashambulizi ya  makombora 18 katika mji mkuu wa Ukraine Jumatatu asubuhi. Ukraine inasema imeyaingilia kati  makombora 15 kati ya hayo. Ripoti za awali kutoka Kyiv ziliashiria  kuwa kulikuwa hakuna vifo, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Pia usiku kucha, Russia iliulenga mji wa mashariki wa Pavlohrad, nchini Ukraine, kwa shambulizi la kombora. Shirika la AP linaripoti kuwa makombora saba yaliulenga mji huo, lakini baadhi yalitunguliwa. Reuters inaripoti kuwa watu 34, wakiwemo watoto watano, walijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo.

Ripoti hiyo iliyokuwa imebandikwa kwenye Twitter, ilisema kuwa kuna picha zinazoonyesha kuwa Russia “imefanya juhudi maalum” kuimarisha mpaka wa kaskazini wa eneo inalolikalia kimabavu la Crimea, “ikiwemo eneo lenye ulinzi karibu na kijiji cha Medvedevka.”

Kulingana na wizara hiyo imeongeza kuwa, Russia imechimba “mahandaki katika eneo la mamia ya maili ndani kabisa ya mpaka wa Russia unaotambuliwa kimataifa, ikiwemo mikoa ya Belgorod na Kursk.

Mahandaki hayo yanaonyesha, taarifa hiyo mpya ilisema, kuwa Russia inahofia kuwa Ukraine inaweza kupata “mafanikio makubwa.”

Baadhi ya shughuli, hata hivyo, wizara hiyo ilisema, “inawezekana ziliamriwa na makamanda wa eneo na viongozi wa kiraia katika jaribio la kuhamasisha maelezo rasmi kuwa Russia “ inatishiwa” na Ukraine na NATO.

Mashambulizi ya Russia kote nchini Ukraine yameua watoto wasiopungua 477 na kuwajeruhi takriban 1,000 tangu Russia ilipoivamia Ukraine zaidi ya mwaka moja uliopita, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine ilisema Jumapili katika ripoti iliyowekwa katika app ya kutuma ujumbe wa Telegram.

XS
SM
MD
LG