Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:22

Russia yaweka kanuni kali koboresha nidhamu ya vikosi vyake Ukraine


Russia imeanzisha hatua kali sana ili kuboresha nidhamu kwa vikosi vyake nchini Ukraine, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Uingereza.

Hatua hiyo imefanyika ikiwa kumefanyika mashambulizi kote Ukraine na kusababisha vifo vya watoto 477 na kujeruhi karibu 1,000 toka Russia ilipofanya uvamizi mwaka mmoja uliopita, ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine imesema Jumapili katika ripoti iliyo chapishwa katika mtandao wa Telegram.

Vifo vingi vimeandikishwa Donetsk na Kharkiv ambapo watu 452, na watoto 275 waliuwawa au kujeruhiwa.

Idadi ya vifo miongoni mwa watoto inatarajiwa kuwa ya juu zaidi ripoti hiyo imesema wakati orodha ya sasa haijajumuisha taarifa kutoka maeneo ambayo yanashikiliwa na Russia ambapo unyama unaendelea.

Jumapili mjini Uman, watoto wawili ambao walifariki katika shambulizi la Ijumaa walizikwa.

XS
SM
MD
LG