Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:27

Ukraine imenasa makombora kadhaa ya Russia


Meli ya Russia ikifyatua makombora Picha: AP
Meli ya Russia ikifyatua makombora Picha: AP

Jeshi la Ukraine limesema kwamba mfumo wake wa ulinzi umezima mashambulizi ya makombora kadhaa ya Russia, leo jumatatu, kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda mkuu wa jeshi amesema kwamba makombora 15 kati ya 18 yaliyorushwa kuelekea mji wa Kyiv yameharibiwa.

Maafisa wamesema hakuna mtu ameuawa wakati wa mashambulizi hayo.

Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba watu 34 wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kuharibiwa.

Vyombo vya habari vya Ukraine vimeripoti kwamba milipuko umetokea katika maeneo ya Dnipro na Sumy.

Russia imeongeza mashambulizi ya makombora dhidi ya Ukraine katika siku chache zilizopita.

XS
SM
MD
LG