Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi. Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara. Gwiji huyo wa Brazil, ambaye jina lake halisi lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia mwaka wa 1958, 1962 na 1970 na anabakia kuwa kinara wa ufungaji wa timu ya taifa akiwa amefunga mabao 77 katika mechi 92 #pele #mfalmewasoka #brazil #ugonjwa #saratani #kombeladunia #bingwa #voa #voaswahili #dunianileo
Matukio
-
Desemba 24, 2024
Waandishi wa habari Msumbiji wanavyopambana taarifa za uongo
-
Desemba 23, 2024
Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara
-
Desemba 20, 2024
Habari Potofu: MISA inawasaidia waandishi Malawi kujenga uaminifu
-
Juni 11, 2024
Je mtu yeyote anaweza kuwa rais wa Marekani?