Juhudi zinazofanywa na kundi la Vijana nchini Burkina Faso wanahamasisha amani, umoja na ustahmilivu kati ya Waislamu na Wakristo wakati wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na Pasaka. Lamina Traore anaripoti kutoka Ouagadougou. Mkamiti Kibayasi anaisoma ripoti kamili.
Sekta ya filamu ya Nigeria, aghlabu hujulikana kama Nollywood, ni watengenezaji wakubwa wa pili wa filamu ulimwenguni kwa kipimo cha wingi wa filamu hizo na inapiga hatua kwa vyote viwili Sanaa na umaarufu katika mauzo ya tiketi.
Nchini Ghana, waganga wa kienyeji, ambao hapo awali waliheshimiwa kama wapatanishi na waponyaji wa kiroho, wanakabiliwa na maswali kuhusu umuhimu wao katika nyakati za sasa.
Ukame, ardhi kugeuka jangwa, ukataji miti na mabadiliko ya hali ya hewa Kaskazini mwa Nigeria yamewalazimisha wafugaji kuhamia kusini wakitafuta maeneo ya malisho kwa mifugo. Harakati hii imepelekea hasara ya zaidi ya maisha elfu 60 kwa mujibu wa spika wa Baraza la Wawakilishi la Nigeria.
[[Ni mtoto wa wazazi kutoka Zimbabwe na Nigeria na hivi leo anahudumu kama mtunukiwa wa cheo cha Naibu Jenerali msimamizi katika kituo cha Mafunzo ya Ukadeti huko Fort Knox, Kentucky. Mwandishi wa VOA Grace Oyenubi anatupasha zaidi kuhusu Brigedia Jenerali Amanda Azubuike, kiongozi wa kijeshi.]]
A Silent War: Ni hadithi za Mateso na Ustahamilivu wa watu nchini Congo” ni makala yenye kukupa shauku kujua zaidi ikiangazia mgogoro wa kibinadamu unaoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hasa eneo la mashariki mwa nchi.