Biden aliwasili Angola Jumatatu kuanza ziara yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu huko Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara na atatumia siku tatu za ziara yake kukabiliana na ushawishi wa China kwa kutangaza mradi wenye matarajio makubwa wa reli unaofadhiliwa na Marekani.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump akiwashukuru wafuasi wake baada ya kuchaguliwa na wananchi kuwa rais wa 47. Trump alikuwa na ujumbe wa kujenga umoja kwa wale waliohudhuria mkusanyiko huo wa mkesha wa matokeo ya uchaguzi huko Florida, Marekani.
Tim Walz, gavana wa Minnesota, amechaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Makamu wa Rais Kamala Harris katika kinyang’anyiro cha kuwania urais. Hizi ni baadhi ya taarifa kuhusu mgombea makamu wa urais kwa tiketi ya Demokratiki. #us #harris #vp #pick #tim #walz #voaswahili
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump wakishiriki katika mdahalo wa CNN wa wagombea urais wa uchaguzi wa mwaka 2024 katika studio za Kituo cha Televisheni cha CNN huko Atlanta, Georgia, Juni 27, 2024.