“Mbali na wanajeshi wa kwanza kutoka Korea Kaskazini waliokamatwa, bila shaka kutakuwa na wengine zaidi. Ni suala la muda tu kabla ya wanajeshi wetu kuweza kuwakamata wengine,” Zelenskiy alisema kwenye mtandao wa X.
Zelenskiy Jumamosi alisema kwamba Ukraine iliwakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini katika mkoa wa Russia wa Kursk, ikiwa mara ya kwanza Ukraine kutangaza kushikwa mateka kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa hai tangu kuingia kwao kwenye vita vya karibu miaka mitatu katika msimu uliopita wa kati ya kipindi cha joto na baridi.
Makadirio ya Ukraine na nchi za Magharibi ni kwamba wanajeshi 11,000 kutoka Korea Kaskazini walipelekwa katika mkoa wa Kursk kuwasaidia wanajeshi wa Russia.
Russia haijathibitisha au kukanusha kuwepo kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini.