Wakati baadhi ya watu wakifurahia hatua hiyo, wanaharakati wa haki wanasema sheria hiyo haijafikia viwango vya kimataifa.
Chini ya Sheria mpya, kila raia anaweza kuomba taarifa ambazo si za siri kutoka serikalini kuhusiana na suala lololote lenye kwa maslahi ya umma.
Msemaji wa Muungano wa Mashirika ya Kiraia ya Zambia au ATI Grant Tungay, amesema sheria mpya haijakamilika, lakini ni mwanzo mzuri.
Sheria mpya ina lengo la kutoa haki ya upatikanaji wa taarifa kama inavyotakiwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya rushwa na mkataba wa Afrika kuhusu haki za binadamu na watu.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, upatikanaji wa taarifa unahamasisha ushiriki wa raia katika utawala, kuwafanya raia waiamini serikali zaidi na kuongeza uhalali wa taasisi za umma