Yale Kenyatta atakayo ibua atakapo kutana na Trump, May

Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta atakutana na viongozi wa Marekani na Uingereza ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mafungamano ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa Kenyatta amefumbia macho matatizo ya kisiasa ambayo viongozi wa Marekani na Uingereza yanawakabili ndani ya nchi zao,

Wanadiplomasia wameliambai gazeti la the Nation kuwa Rais Kenyatta katika ziara yake ya Washington, Jumapili, atakuwa anatafuta uwezekano wa nchi yake kuyafikia masoko na kupata nyenzo ya kuwanyanyua wazalishaji wadogo wadogo nchini Kenya, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya nchi hiyo katika kuboresha sekta ya viwanda.

Siku ya Jumatatu, Rais Kenyatta amepangiwa kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump White House, ikiwa ni mkutano wa ushirikiano kati ya pande mbili wa kwanza kufanyika Marekani kati ya nchi hizo mbili.

Baadae Rais atampokea Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May huko mjini Nairobi Alhamisi. Mikutano yote hiyo imeweka kipaumbele katika ushirikiano wa biashara, uwekezaji na usalama wa eneo.