Winnie alikuwa anatibiwa figo iliyokuwa ina matatizo, msemaji wa familia ya Mandela amesema katika tamko lake.
Madikizela-Mandela alilazwa katika hospitali ya Milpark Johannesburg siku 10 zilizopita. Amekuwa akipokelewa hospitalini na kuruhusiwa tangu mwaka 2016 kwa matibabu ya mgongo na goti.
“Nimefurahi kuruhusiwa kwenda nyumbani ambapo nitaweza kupumzika na kurejesha kikamilifu hali yangu kutokana na maradhi ya muda mfupi,” tamko hilo limemkariri Madikizela-Mandela.
Wakati mtalaka wake alipokuwa anatumikia kifungo cha miaka 27 kwa ajili ya kupinga ubaguzi wa rangi , Madikizela-Mandela alifanya kampeni kushinikiza atolewe jela na kupigia kelele haki za Waafrika weusi nchi Afrika Kusini, na alikamatwa na kupigwa marufuku nchini. Utawala wa wazungu wachache ulifikia kikomo mwaka 1994.