Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:24

Mkutano wa viongozi wa Afrika wazingatia vita dhidi ya rushwa


Viongozi wa AU wazingatia vita dhidi ya rushwa wanapokutana Addis Ababa
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00

Mkutano wa 30 wa viongozi wa Umoja wa Afrika umeanza mjini Addis Ababa siku ya Jumapili kukiwa na wito wa kuanzishwa kwa eneo la biashara huru barani Afrika pamoja na kuzingatia mageuzi ya umoja huo na vita dhidi ya ulaji rushwa.

Mwenyekiti mpya wa Umoja huo kwa mwaka huu Rais Paul Kagame wa Rwanda alisisitiza juu ya swala hilo katika hotuba yake ya ufunguzi.

“Hii leo tutazindua soko la pamoja la Afrika la usafiri wa anga. Hii ikiwa ni hatua muhimu kuendelea mbele katika usafiri. Na tuko karibu ya kuidhinisha eneo la soko huru barani huku. Kwa hakika inahitaji kuanza kutekelezwa mwaka huu.” Alisema Rais Kagame.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kuimarisha umoja wa waafrika kwanza.

“Kutokana na kuongezeka hali ya ubinafsi wa kitaifa, kuzuka chuki dhidi ya wageni na kuwakata watu wengine ni isahara kamili kwamba misingi ya umoja, usawa na haki inaanza kuporomoka. Kwa hivyo tukikabiliwa na hali hii inayotia wasiwasi tunatoa wito wa kuimarisha umoja, kustahmiliana na kuheshimiana.” amesema Mahamat

Marais na wakuu wa serikali kutoka mataifa 54 walizungumzia haja ya dharura ya kupambana na mashambulizi ya kigaidi ambayo yameanza kua kitisho kikubwa kwa amani, usalama na maendeleo barani humo .

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika kikao cha ufunguzi amekisifu kikosi cha pamoja cha mataifa ya G5 ya Sahel kwa kuanza kukabiliana na itikadi kali katika kanda yao.

“Kikosi cha pamoja cha Sahel cha G5 kinakabiliana na ugaidi, ukosefu wa usalama, biashra haramu ya binadamu na dawa za kulevya katika kanda yao. Na kikosi cha pamoja ya mchanganyiko wa mataifa kinapambana na Boko Harana, ugaidi katika kanda ya ziwa Chad. Lakini operesheni hizi zinahitaji uungaji mkono kutoka jumuia ya kimataifa.”

Katika kikao maalum siku ya Jumamosi usiku, cha baraza la Usalama na Amani la AU viongozi wa Afrika walijadili miongoni mwa maswala mengine amani ya Afrika, hali ya vita Sudan Kusini, namwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Faki Mahamat alisema, wakati umefika kuwawekea vikwazo wale wanaozuia kupatikana amani katika taifa hilo.

Marekani mfadhili mkubwa wa msaada kwa Sudan Kusini kwa mara nyingine tena imetoa wito wa vikwazo vya silaha viwekewe Juba wakati wa mkutano wa baraza l;a usalama la umoja wa mataifa wiki ilyiopita. Mkutano huo wa viongozi unaomalizika Jumatatu utazingatia zaidi juu ya namna ya kushinda vita dhidi ya rushwa

XS
SM
MD
LG