WHO yatadharisha uwezekano wa kuendelea virusi vya corona daima

Wafanyakazi wanatengeneza barakoa kiwandani wakati ugonjwa wa corona ukishika kasi mjini Gunung Putri, Bogor karibu na Jiji la Jakarta, 15 April 2020. photo taken by Antara Foto. Antara Foto/Yulius Satria Wijaya/ via REUTERS ATTENTION EDITORS(Foto: Antara via Reuters)

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetahadharisha uwezekano wa kuendelea virusi vya corona vikaendelea kuwepo daima.

Mkurugenzi wa masuala ya dharura WHO, Det Mike Ryan, ametahadharisha dhidi ya utabiri kuhusu uwezekano wa virusi hivyo kutokomezwa kabisa.

Amesema hata kama chanjo dhidi ya virusi hivyo itapatikana, juhudi kubwa zitahitajika kukabiliana na virusi hivyo.

Karibu watu milioni 4.3 wameambukizwa virusi vya corona, na 300,000 wamefariki kwa mujibu wa hisabu ya janga hilo duniani.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa (UN) umeonya kwamba janga la virusi vya corona linaendelea kusababisha matatizo ya kiakili na msongo wa mawazo, hasa katika nchi ambazo kuna sekta dhaifu za afya.

UN inahimiza serikali mbalimbali kuzingatia afya ya akili kama sehemu ya kukabiliana na athari zinazo sababishwa na virusi vya corona.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.