White House yafafanua tamko la Trump dhidi ya Obama

Sean Spicer

Idara ya Sheria imeomba kupewa muda zaidi kujibu agizo la Bunge la Marekani linaloitaka ipeleke ushahidi juu ya madai ya Rais Donald Trump dhidi ya Rais mstaafu Barack Obama, kwamba alirikodi simu zake New York, wakati wa kampeni.

Trump hakutoa ushahidi wowote wakati alipotuma madai hayo katika ujumbe wa tweeter mapema mwezi huu.

Lakinimsemaji wa White House Sean Spicer amesema Trump hakukusudia kwamba Obama alirikodi simu yake.

Akizungumza Jumatatu katika mkutano na waandishi White House, Spicer alikuwa anajaribu kusawazisha tamko lilotolewa na rais kupitia ujumbe wa Twitter likidai kuwa Obama aliamrisha uchunguzi wa Hoteli yake ya New York City hotel.

“Sio kwamba anafikiria kuwa Rais Obama alikwenda na kurikodi simu yake yeye mwenyewe,” Spicer amesema.

Trump aliamsha hisia za wengi mapema wiki hii pale alipotuma tweet: “Je ni sheria kwa Rais alioko madarakani “kurikodi” mbio za kugombea urais kabla ya uchaguzi? Lililotupiliwa mbali na mahakama hapo awali… Sheria mpya !”

Katika tweet nyingine baadae, Trump ameandika: Ninaweza kuweka dau kwamba wakili yoyote mzuri anaweza kutengeneza kesi nzuri kutokana na ukweli kwamba, Rais Obama alikuwa anarikodi simu zangu mwezi wa Oktoba, kabla tu ya uchaguzi!’