Waziri wa Fedha wa zamani wa Afrika Kusini afariki dunia

Waziri wa Fedha wa zamani wa Afrika Kusini Tito Mboweni, akiwa kwenye mkutano mjini Cape Town, OOktoba 30, 2019. REUTERS/Sumaya Hisham -/Picha ya maktaba.

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema Jumapili kwamba waziri wa zamani wa Fedha na Kazi ambaye pia alikuwa gavana wa kwanza mweusi wa Benki Kuu, Tito Mboweni, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mboweni alikuwa mwanaharakati dhidi ya utawala wa kibeberu akiwa mwanafunzi wakati huo, na kisha baadaye kuwa waziri wa kwanza wa Kazi kuanzia 1994, hadi 1999, wakati wa utawala wa Rais Nelson Mandela. Baadaye alihudumu kama Gavana wa Benki Kuu kwa muongo mmoja kuanzia 1999, na kisha kuwa waziri wa fedha kuanzia 2018, hadi 2021, chini ya Rais Cyril Ramaphosa.

Chama chake ya ANC kimesema kuwa mchango wake katika kuleta demokrasia nchini humo katika siku za mwisho mwisho za ubeberu hauwezi kusahaulika. Mboweni alisaidia katika kuleta sheria za wafanyakazi baada ya uhuru ambazo ziliwapa sauti wafanyakazi, pamoja na kulinda haki zao. Mboweni alikuwa mtu wa karibu na Ramaphosa na alihudumu kwenye Kamati Kuu ya Kitaifa ya ANC, ambayo hufanya maamuzi muhimu ya kisiasa ndani ya chama hicho.