Waziri wa Afghanistan anayehusika na wakimbizi auawa katika mlipuko

Waziri wa Afghanistan anayehusika na wakimbizi Khalil Ur-Rahman Haqqani.

Waziri wa Afghanistan anayehusika na wakimbizi aliuawa Jumatano katika mlipuko kwenye afisi za wizara hiyo katika mji mkuu Kabul, chanzo cha serikali kimeiambia AFP.

“Kwa bahati mbaya, milipuko ulitokea kwenye wizara ya wakimbizi na waziri Khalil Ur-Rahman Haqqani ameuawa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake,” afisa wa serikali amesema, kwa masharti ya kutotajwa jina.

Khalil Ur-Rahman Haqqani alikuwa kaka wa Jalaluddin Haqqani, ambaye alianzisha mtandao wa Haqqani uliohusika katika baadhi ya mashambulizi mabaya wakati wa uasi wa miongo miwili wa Taliban.

Alikuwa pia mjomba wa Sirajuddin Haqqani, waziri wa sasa wa mambo ya ndani.