Jeshi la Sudan, ambalo limekuwa likipigana na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) tangu Aprili 2023, Limeweza kusonga mbele kuelekea mji mkuu katika wiki za hivi karibuni, kwa lengo la kuudhibiti tena mji wa Khartoum.
Jumapili, kituo cha mafuta katika eneo la kusini mwa Khartoum linalodhibitiwa na RSF kilishambuliwa kwa makombora, limesema kundi la The South Belt Emergency Response Room.
Kundi hilo la kujitolea linaloongozwa na vijana limesema “watu 28 wamethibitishwa kufariki” na idadi ya waliojeruhuwa imefikia 37, ikiwa ni pamoja na 29 walioungua moto” na baadhi wana majeraha mabaya.