Siku moja baada ya shambulizi wakazi walionekana wakitafuta mali katika vifusi vya majengo yaliyoanguka.
Akizungumza na shirika la Habari la Reuters, Meya Majed Drbes alisema mashambulizi hayo, ambayo yalilenga sehemu ya kaskazini kabisa mwa Lebanon iliyopigwa na wanajeshi wa Israel tangu mapigano yalipoanza Oktoba 2023, yalipiga jengo ambalo watu 30 walikuwa wakiishi wakiwemo wakimbizi wa Syria, huku baadhi ya watu wakiwa wamekwama chini ya vifusi.
Jeshi la Israel lilisema kuwa vikosi vyake vililenga jengo la kijeshi lililokuwa na magaidi kufuatia taarifa za uhakika za kijasusi na kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa wasio na hatia na kuongeza kuwa ripoti za majeruhi hazikuwa sahihi.
Mapema Jumatatu, uvamizi wa Israel huko Al-Saksakieh katika Wilaya ya Sidon iliua takriban watu saba na kuwajeruhi wengine saba kulingana na wizara ya afya ya Lebanon.