“Shambulio lilifanyika Jumamosi usiku na kwa bahati mbaya tulipoteza raia sita, alisema Augustin Kapupa, afisa katika mtaa wa Matembo ambako shambulio la kwanza lilifanyika.
Kapupa amewatuhumu waasi wa ADF kuhusika na shambulio hilo, kihistoria likiwa kundi linaloundwa na muungano wa waasi wengi wao wakiwa Waislamu na ambalo lilianzishwa mashariki mwa DRC mwaka wa 1995.
Wafuasi wake wameua maelfu ya raia tangu wakati huo.
Kundi hilo, moja ya makundi ya wanamgambo yanayotekeleza mauaji mabaya katika eneo hilo lenye mzozo, lilitangaza kuwa chini ya uongozi wa kundi la Islamic State mwaka wa 2019.
“Baada ya mauaji ya ADF huko Matembo, walitujia hapa Sayo, na kutuacha tukiomboleza vifo vya watu watano,” alisema mkuu wa eneo hilo Antoine Kambale.
Afisa wa Beni, Makofu Bukuku aliiambia AFP kwamba idadi ya vifo huko Sayo inaweza kuongezeka, kwa sababu waasi bado wapo katika eneo hilo.
Bukuku amesema alitumai kwamba jeshi la Congo katika eneo hilo, pamoja na wanajeshi wa Uganda na kuwepo kwa kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO, ilikuwa inatosha kuwaepusha na hatari ya mara kwa mara.
“Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, tumerekodi vifo na utekaji nyara tu,” alisema.