Katika eneo la Rafah lililopo Kusini mwa Gaza, linalopakana na Misri lilikuwa ni eneo pekee katika eneo zima la sehemu ya Palestina kupokea misaada kiasi katika kipindi cha siku nne. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Misaada ya Kibinaadamu ilisema siku ya Alhamisi.
Lakini bado hakuna chakula cha kutosha kwa kila mtu na wazazi wamesema watoto wao wameanza kuugua na wanapungua uzito. Wakiwa wamekaa kwenye mkeka mbele ya hema la familia katika kambi ya muda kwa waliopoteza makazi, Zakaria Rehan akiwa amembeba mtoto wake wa kiume Yazan, akimnywesha maziwa kidogo ya kopo yaliyokuwemo. “Haya ni maji tu yametiwa kijiko kimoja cha maziwa, inawezekana hata hakikufika kijiko kizima, chochote kile ili yanukie kama maziwa” Ili niweze tu kumfanya afikirie kuwa ni maziwa ili aweze kunywa” alisema Rehan.
“Lakini si afya, hayampatii virutubisho vyovyote”
Rehan amesema familia zote zilizoko katika kambi hiyo zinahangaika kutafuta chakula na jinsi ya kupika kila siku. Amesema amekuwa akila maharage mabichi ya kopo yaliyopelekwa kwa njia ya msaada kwa sababu hakuna mafuta ya kuyapasha moto.
Uhaba wa chakula umekuwa tatizo kwa kipindi kizima cha miezi miwili ya vita vya muda mrefu kati ya Israel na Hamas, Lakini tatizo hilo limezidi tangu kumalizika kwa wiki ndefu ya mwezi Desemba ya makubaliano ya usitishwaji vita. Wakati idadi ya malori ya misaada yanayoingia yakitokea Misri yakiwa yamepungua na usambazaji ukiwa unachelewa kutokana na mapigano makali yakiwemo ya Kusini mwa Gaza.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters