Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:35

Marekani imeweka marufuku ya Visa kwa walowezi wa Israel


Logo ya Visa ya Marekani
Logo ya Visa ya Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje imetangaza Jumanne kwamba  inaanza kuweka marufuku ya kusafiri kwa darzeni ya walowezi wa Kiyahudi wenye msimamo mkali katika eneo linalokabiliwa kimabavu huko Ukingo wa Magharibi

Marekani imeweka marufuku ya visa kwa walowezi wa Israel waliojihusisha na ghasia huko Ukingo wa Magharibi dhidi ya Wapalestina.

Wizara ya Mambo ya Nje imetangaza siku ya Jumanne kwamba inaanza kuweka marufuku ya kusafiri kwa darzeni ya walowezi wa Kiyahudi wenye msimamo mkali katika eneo linalokabiliwa kimabavu huko Ukingo wa Magharibi ambao wamehusishwa na mfululizo wa mashambulizi ya karibuni.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mathew Miller anasema hatua inachukuliwa hivi sasa kwasababu serikali ya Israel haijachukua hatua za kutosha ili kuzima ghasia kama hizo, ambazo zilisambaa baada ya kundi la kigaidi la Hamas kuwashambulia raiai wa Israeli hapo Oktoba 7.

Miller anasema “Tumeelezea bayana kwamba tunadhani ukweli unaunga mkono walichofanya, watu ni lazima wachukuliwe hatua kama wametenda vitendo yvya ghasia. Na hivyo, tumechukua hatua kwamba sisi, kama serikali ya Marekani tunaweza kuchukua. Hiyo haizuii haja kwa serikali ya Israel kuchukua hatua zake mwenyewe, na tutaendelea kuwa wazi na wao.”

Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken, katika taarifa yake, amesema Marekani itaendelea kuwawajibisha walowezi kwa ghasia dhidi ya Wapalestinaz, pamoja na mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya Waisraeli, hasawakati ambapo mivutano iko juu mno kutokana na vita kati ya Israel na Hamas huko Ukanda wa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG