Watoto milioni 400 wanyanyaswa kingono duniani - Ripoti ya Economist Impact

Simone Biles and Aly Raisman wakikumbatiana baada ya Seneti Marekani kusikiliza ripoti ya uchunguzi wa FBI kuhusu kesi ya Larry Nassar, Jumatano, Septemba 15, 2021 in Washington. Nassar alishitakiwa kwa makosa ya picha za ngono na unyanyasaji wa kingono huko Michegan 2016.

Kila mwaka, watoto zaidi ya millioni 400  duniani  wananyanyaswa  kingono, ripoti mpya  ya Enonomist Impact imesema.

Kwa kawaida ukatili na unyanyasaji kingono hufanywa siri kwa kuhofia aibu na kunyanyapaliwa, hivyo kuruhusu uhalifu huo kuendelea.

Ripoti hiyo “Out of the Shadows Global Index 2022” inaonyesha kuwa wakati baadhi ya nchi za Afrika zimeweka mifumo imara ya kushughulikia ukatili na unyanyasaji wa watoto kingono, mifumo hiyo huanza kufanya kazi baada ya mtoto kuathirika kwa hiyo haiwalindi watoto dhidi ya waharibifu.

Nchi 60 zilizofanyiwa utafiti zina asilimia 85 ya idadi ya watoto duniani. Uingereza, Ufaransa na Sweden zimepata alama ya juu kuwa na mifumo mizuri ya kulinda na kushughulikia unyanyasaji wa watoto.

Vipimo vilivyotumika kupitia nguzo tano za kuzuia na kushugulikia unayanyasaji wa watoto: sheria za kuwalinda; Sera na mipango; uwezo wa taifa na utayari; huduma za usaidizi na mchakato wa utoaji wa haki katika nchi mbalimbali.

Kwa Africa, Afrika ya Kusini zilikuwa kati ya nchi bora 20 ambazo zina sera zenye mafanikio. Afrika ya Kusini ni nchi pekee iliyoko kwenye kundi la kumi bora kwa aina zote tano za vipimo hivyo, na kuwa mfano mzuri wa mbinu kamilifu za kulishughulikia suala hili la ukatili na unyanyasaji wa watoto kingono.

Ni moja ya nchi kumi ambazo zina mahakama maalumu za kushughulikia kesi za unyanyasaji kingono, na moja kati ya nchi mbili zenye sheria kamili zinazotetea waathirika walionusurika, ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya kutowaadhibu waathirika wa biashara haramu ya watoto.

“Ni muhimu, na pia imeondoa sheria ya kuweka kikomo cha muda kwa kesi za ukatili na unyanyasaji kingono kwa watoto, ili kutoa nafasi ya kesi nyingi zaidi kuripotiwa” ripoti hiyo imesema.

Kwa Afrika Mashariki, Kenya imeshika nafasi ya 21 wakati Rwanda imeshika nafasi ya 27 na Tanzania ya 33.

Akizumgumzia udhaifu ulioonyeshwa na nchi za Afrika Mashariki, mashirika yanayoshughulikia haki za watoto yamekubali kuwa utekelezaji wa sheria bado ni changamoto.

Habari hii imetoka kwenye gazeti la The East Africa