Wataalamu waonya uognjwa wa ‘Monkey Pox’ utawafanya mashoga kubaguliwa DRC

Wanaharakati nchini Kenya wakiadhimisha siku ya Kimataifa ya Kuutokomeza umaskini huko Nairobi, tarehe 17 Januari 2020. Picha na TONY KARUMBA / AFP

Wakati Congo inakabiliana na ongezeko kubwa sana la mlipuko wa ugonjwa wa monkey pox, wanasayansi wanaonya juu ya ubaguzi dhidi ya mashoga na wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mwezi Novemba, Shirika la Afya Duniani limeripoti kuwa ugonjwa wa mpox ambao pia unajulikana kama monkey pox, umekuwa ukisambaa kwa njia ya ngono huko Congo kwa mara ya kwanza.

Ugonjwa wa mpox umekuwepo katika sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi kwa miongo kadhaa, lakini ilikuwa mpaka mwaka 2022 ulipothibitishwa kusambaa kwa njia ya ngono; wengi walioambukizwa katika takriban nchi 100 mwaka huu walikuwa mashoga au wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia zote.

Huko Afrika, kutoridhia kwa ripoti kuhusu dalili kunaweza kusababisha ongezeko la maambukizi ya chini kwa chini, alisema Dimie Ogoina ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo kikuu cha Delta nchini Nigeria. “Inawezekana kwasababu mahusiano ya jinsia moja yamepigwa marufuku na sheria katika sehemu nyingi za Afrika, watu wengi hawajitokezi kama wanadhani wameambukia mpox” alisema Ogoina.

Maafisa wa WHO wamesema, waligundua visa vya kwanza vya maambukizi kwa njia ya ngono,katika kesi mbaya za kwanza za ugonjwa wa mpox huko Congo majira ya kipupwe yaliyopita, muda mfupi baada ya mkaazi wa Ubelgiji ambaye “ alijitambulisha kama mwanamme mwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine” alipowasili Kinshasa, mji mkuu wa DRC.

Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba Congo inashukiwa kuwa na kesi 13,350 za mpox, vikiwemo vifo 607, na asilimia kumi ya kesi hizo zimethibitishwa na maabara.

Lakini haijafahamika ni maambukizi mangapi ni ya njia ya ngono.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP