Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema Jumanne kwamba mapigano upande wa magharibi ya Sudan katika jimbo la Darfur yameongezeka na kufikia “kiwango cha kushtusha.”
Vita hivi vimewasababisha Wasudan wengi kutokua na hamu ya kuchinja kondoo au mnyama mwengine kama ilivyo desturi katika siku hii muhimu kwa waislamu kutoa sadaka kwa watu wenye mapato ya chini katika jamii.
Mzozo huo ambao sasa upo katika mwezi wa tatu, umesababisha vifo na vurugu nchini pamoja na kusababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao katika nchi hiyo ambayo tayari ilikuwa ikikabiliwa na umaskini kabla ya mapigano hayo kuzuka.
Kama walivyo kwa wakazi wengi wa Khartoum, Hanan Adam alikimbia na watoto wake sita wakati vita vilipozuka katikati ya mwezi Aprili kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha dharua (RSF).
Kwa sasa anaishi katika kambi ya muda iliyoko kusini mwa jiji, familia yake ikijaribu kusherehekea sikukuu ya Eid mbali na nyumbani na bila furaha.
"Katika mzingira haya, sikuu ya Eid haitakuwa na furaha," Adam aliliambia shirika la AFP kutoka kambi ya Al-Hasaheisa, iliyopo takriban kilomita 120 kutoka Khartoum.
Hakuna siku inayopita bila watoto wake, wenye umri wa kati ya miaka miwili na 15, kumuuliza ni lini watarudi nyumbani, alisema.
Kabla ya mzozo kuanza, thuluthi mbili ya wakazi wa Sudan walikuwa wanaishi katika umaskini uliokithiri, na kati ya watu watatu mmoja anategemea misaada ya dharura ili kujikimu kimaisha, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.