Wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza, wameitaka Russia kupunguza hali ya wasiwasi kuhusu Ukraine na kuchukua hatua za kidiplomasia, wakati maelfu ya wanajeshi wa Russia wanajiandaa mjini Belarus kama sehemu ya kuongeza idadi yao kwenye mpaka na Ukraine.
Katika kikao na Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov, Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Liz Truss, ameonya Russia kwamba hatua ya kuishambulia Jirani wake itaisababishia athari kubwa sana na itakuwa na gharama ghali sana.
Truss ametaka utawala wa Moscow kupunguza hali ya mvutano na wasiwasi na kuheshimu mikataba yake ya kimataifa kuhusu uhuru na hali ya Ukraine kujitawala yenyewe.
Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergrey Lavrov, amesisitiza kwamba Moscow haitakubali shinkizo za mataifa ya magharibi.
Mkutano kati ya Truss na Lavrov ni wa kwanza katika mda wa zaidi ya miaka minne.