Mwendesha mkuu wa mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Bw Luis Moreno-Ocampo amefikisha mbele ya mahakama Jumatano, majina ya watu 6 raia wa Kenya ikiwa ni pamoja na maafisa wa juu wanaoshukiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Washukiwa waliotajwa leo ni pamoja na naibu waziri mkuu ambae ni waziri wa fedha Uhuru Kenyatta, waziri wa zamani wa elimu William Rutto, na waziri wa viwanda Henry Kosgey.
Wengine ni mkuu wa zamani wa Polisi Mohamed Hussein Ali, mwandishi wa habari Joshua Arap Sang na katibu wa baraza la mawaziri Francis Muthaura .
ICC lazima iamue kama itawafungulie mashitaka washukiwa hao, baada ya uchunguzi wa kina.
Ocampo amesema washukiwa hao wanafikiriwa kuwa wanahusika zaidi na ghasia zilzopelekea watu 1300 kupoteza maisha yao.