Wapiganaji kadhaa wa Islamic State waripotiwa kuuawa katika jimbo la Somalia la Puntland

Ramani ya jimbo la Somalia la Puntland

Maafisa wa usalama nchini Somalia wamesema waliwauwa wapiganaji kadhaa wa kundi la Islamic State na kuteka vituo vinane vya wanajihadi wakati wa operesheni ya kijeshi inayoendelea katika jimbo huru la Puntland.

Islamic State ina idadi ndogo ya wapiganaji nchini Somalia ikilinganishwa na kundi la Al-Shabaab lenye uhusiano na Al-Qaeda, lakini wataalam wameonya kuwa IS imeongeza harakati zake.

Afisa wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na ugaidi alionya mwaka jana kuhusu kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi yenye uhusiano na Islamic State nchini Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Somalia.

Maafisa wa Somalia Jumatatu walisema operesheni katika mkoa wa kaskazini ilifanyika zaidi karibu na milima ya Cal Miskat katika jimbo la Bari.

“Vikosi vya usalama vilichukua udhibiti wa vituo vinane vya jeshi la IS ikiwemo kimoja muhimu katika milima ya Cal Miskat. Watu kadhaa wenye silaha wakiwemo wapiganaji wa kigeni waliuawa katika operesheni za kijeshi”, jeshi la Puntland lilisema katika taarifa.