Waokoaji waendelea kuwasaka waathirika wa tetemeko Uturuki

Watu wasiopungua 27 wamefariki katika tetemeko la ardhi lililotokea Ijumaa nchini Uturuki huku wengine zaidi ya 800 wakijeruhiwa. Timu ya uokozi ikimuondoa msichana wa miaka 7 aliyeokolewa kutoka katika jengo lililoanguka huko mkoa wa Izmir, Uturuki, Jumamosi.

Timu za uokozi zinatafuta katika vinatafuta katika simenti na vifusi vya majengo nane yaliyoanguka leo Jumamosi wakiwasaka walionusurika katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki.

Tetemeko hilo kubwa la ardhi ambalo limepiga pwani ya Aegean nchini humo na kisiwa cha Samos kilichopo kaskazini mwa Ugiriki Ijumaa kimesababisha vifo vya takriban watu 27.

Zaidi ya watu 800 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko hilo ambalo liliangusha majengo huko Izmir mji wa tatu kwa ukubwa nchini Uturuki, na kuchochea dhoruba ndogo ya tsnumani katika wilaya ya Saferihisar na huko Samos.

Tetemeko ambalo taasisi ya Kandili imesema lilikuwa katika kiwango cha 6.9 kwa kipimo cha rikta ilipiga jana mchana kwa saa za Uturuki, hasa katika maeneo ya Aegean kaskazini mashariki mwa Samos. Tetemeko hilo lilifuatia na mitetemeko kadhaa midogo zaidi ya 400.

Gavana wa Izmir Yavus Selim Kosger amesema sio chini ya watu 70 waliokolewa kutoka katika kifusi cha jengo lililobomoka na katika majengo mengine 10 yalioanguka.

Wakati tetemeko likitokea wakazi walionekana wakikimbia mitaani katika mkoa wa Izmir wenye wakazi milioni 4, wakiwa wamefazaika.

Aidha, tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa kipimo cha Richter 7.0,

Tetemeko hilo lilisababisha maji mengi kuingia katika wilaya ya Seferihisar, mkoani Izmir.

Katika nchi jirani ya kisiwa cha Ugiriki cha Samos, mvulana na msichana walikutwa wamefariki katika eneo ambalo ukuta ulianguka.

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kila kinachowezekana kitafanyika ambacho ni muhimu kusaidia juhudi za uokoaji.