Wananchi wa Chad Jumatatu wamepiga kura katika uchaguzi wenye lengo la kumaliza miaka mitatu ya utawala wa kijeshi lakini uliosusiwa na wapinzani wa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby.
Wataamua ikiwa wanataka kuongeza miongo mitatu ya utawala wa familia ya Deby, katika nchi hiyo muhimu katika vita dhidi ya uasi wa wanajihadi katika eneo la jangwa la Sahel.
Mpinzani mkuu kwenye kinyang’anyiro cha rais ni waziri mkuu Succes Masra, anayeshtumiwa na wakosoaji kuwa kibaraka kwa kutokuwepo wapinzani wengine wakubwa.
Wagombea wote wawili wameapa kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, ambao mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yanaonya kuwa hautakuwa huru au wa haki