Mabadiliko ya maoni haya yanasukumwa zaidi na ongezeko la hofu kati ya Warepublikan, wakati Wademokratiki wanaendelea kuona faida mbalimbali zinazoletwa na wahamiaji, ukusanyaji maoni mpya unaonyesha.
Ukusanyaji maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha shirika la AP- NORC Center for Public Affairs kimegundua kuwa idadi kubwa ya watu wazima Marekani wanaamini kuwa wahamiaji wanachangia katika ukuaji wa uchumi na wanatoa michango muhimu kwa utamaduni wa Marekani.
Lakini inapokuja kwa wahamiaji halali, watu wazima Marekani wanaona faida kubwa chache kuliko walivyo kuwa wakiona huko siku za nyuma, na zaidi ni hatari kubwa.
Wamarekani 4 kati ya 10 wanasema kuwa wahamiaji wanaokuja Marekani kisheria, ni faida kubwa kwa makampuni ya Kimarekani kupata utaalamu wa wafanyakazi wenye mafunzo katika fani kama vile sayansi na teknolojia.
Hivyo hivyo asilimia 38 walioshiriki wanasema kuwa wahamiaji halali wanachangia faida kubwa kwa kukuza utamaduni na maadili ya Marekani.
Lakini hesabu hizo zimeteremka ukilinganisha na utafiti wa 2017, ambapo Wamarekani asilimia 59 walisema wafanyakazi wahamiaji wenye ujuzi wanaoingia nchini kisheria ni faida kubwa, na nusu ya hao walisema wahamiaji halali wanachangia faida kubwa kwa kukuza utamaduni wa Marekani.
Wakati huo huo, Wamarekani waliochangia katika utafiti huo wanasema kuwa kuna ongezeko la hatari kubwa ya wahamiaji halali kufanya vitendo vya uhalifu nchini Marekani, hisia hiyo ikiwa imepanda kutoka asilimia 19 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 32 katika utafiti huu mpya wa maoni.
Warepublikan walikuwa ni rahisi zaidi kusema uhamiaji ni suala muhimu kwao binafsi kuliko Wademokrat, na asilimia 41 hivi sasa wanasema ni hatari kubwa ilivyokuwa wahamiaji halali watafanya vitendo vya uhalifu Marekani, idadi hiyo imeongezeka kutoka asilimia 20, 2017.
Kwa ujumla, Warepublikan wanatarajiwa zaidi kuona hatari kubwa mbalimbali – na faida finyu zaidi – kutoka kwa wahamiaji ambao wanaingia nchini kwa kufuata sheria na wale wanaoingia kinyume cha sheria, ingawa wanakuwa zaidi na wasiwasi kuhusu watu ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.