Shirika la kutetea haki za binadamu – Human Rights Watch, limewashutumu walinzi wa mpakani wa Saudi Arabia kwa kuua mamia ya wahamiaji wa kiuchumi wa Ethiopia.
Wahamiaji hao walikuwa wakijaribu kuvuka mapakani kutoka kwenye taifa lililokumbwa na vita la Yemen.
HRW imesema takriban watu 655 wameuwawa na walinzi tangu mwanzoni mwa 2023 kwa kupigwa risasi wakati wengine wakijeruhiwa kutokana na milipuko.
Shirika hilo limetumia miezi kadhaa kukusanya ushahidi baada ya Umoja wa Mataifa, UN, kutoa shutuma kama hizo mwaka 2022.
HRW imeyaita mauaji hayo yaliyoenea na yaliyopangiliwa, yanaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Mwezi Machi serikali ya Saudi Arabia ilikataa pendekezo lolote kwamba wanajeshi wake walihusika na mauaji ya watu waliotaka kukatisha mpaka.
Habari hii inatokana na mashirika mbalimbali ya habari.