Waandamanaji hao walilenga maafisa, akiwemo mkuu wa bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa nchi, Aguila Saleh, walipokusanyika nje ya Msikiti wa Sahaba.
Wengine waliketi juu ya paa la jengoi la jengo la bunge, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Baadaye jioni, waandamanaji wenye hasira walichoma moto nyumba ya aliyekuwa meya wa mji wa Derna wakati wa mafuriko hayo, Abdulmenam al-Ghaithi, meneja wa ofisi yake aliliambia shirika la habari la Reuters.
Reuters haikuweza mara moja kumfikia Ghaithi kwa maoni yake.
Maandamano ya Jumatatu ndiyo ya kwanza tangu mafuriko hayo, ambayo ambayo yalibebe vitongozi vizima, hasa baada ya mabwawa mawili kuvunja kingo katika moja ya mikasa mibaya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo.