Mahujaji kutoka ulimwenguni kote walifurika Ijumaa katika maeneo mbalimbali kupitia njia finyu zilizoko eneo la Cobblestone wakipitia eneo la Dolorosa katika mji wa zamani wa Jerusalem ili kushiriki katika maandamano ya sherehe za Ijumaa Kuu.
Wamekuwa wakiimba nyimbo za kiroho na kusoma baadhi ya vifungu vya Bibilia, wakifuatilia nyao za Yesu hadi kufika katika vituo 14 vya msalabani.
“Bila shaka niheshima kubwa kwangu kuwa katika ardhi hii tukufu kwa maadhimisho haya. Ni kitu kikubwa sana. Inanisaidia katika imani yangu, inanisaidia katika kila kitu,” amesema Gary Osterberg anaetokea Canada.
Katika ardhi hiyo takatifu, dini na siasa havigawanyiki. Sikukuu ya Pasaka imekuja wiki sita kabla ya mpango wa Marekani kuhamisha ubalozi wake huko Israel kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
“Nafikiri kuwa kuhamisha kwa ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem ni jambo sahihi. Nafikiri ni kitu muwafaka kufanyika. Na natamani kama Canada ingefuata hilo na kutekeleza uhamisho huo; kuhamisha Ubalozi wa Canada kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
Lakini Wapalestina wamekasirishwa na hatua hiyo ya kuhamisha ubalozi na uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kama makao makuu ya Israel. Imad, muuza duka katika soko la Arab bazaar, amesema anatarajia siku za usoni kuwaJerusalem itakuwamji mkuu wa Palestina
“Sitarajii kitu chochote kutoka kwa Donald Trump, bali vitu vibaya. Hili, unafahamu, ni sehemu ya yale ambayo wanayafanya dhidi ya Wapalestina: hatua nyingine, kitu kingine, ambacho kitawaumiza Wapalestina.”