Wakati Russia ikizidisha mashambulizi, Marekani yatoa msaada mpya kwa Ukraine

Your browser doesn’t support HTML5

Russia inapoendelea kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, Rais wa  Marekani analiomba Bunge la Marekani Alhamisi kuidhinisha msaada mpya kwa ajili ya Jeshi la Ukraine.

Ukraine imesema kwamba mashambulizi ya Russia mashariki mwa nchi hiyo yameongezeka sana, huku miji kadhaa ikishambuliwa katika jaribio la wanajeshi wa Russia kutaka kuwazingira wanajeshi wa Ukraine.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema Marekani itatoa msaada wa zaidi ya dola milioni 200 kwa Pembe ya Afrika. Msaada huo utajikita katika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu yanayosababishwa na ukame na mzozo wa kikanda.

Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari