Wahamiaji wa Afrika Magharibi wamegunduliwa wamefariki ndani ya boti ambayo ilikuwa imepoteza muelekeo huko Cape Varde, pamoja na manusura takriban 40.
Afrika —
Hata hivyo idadi kamili ya waliofariki haijathibitishwa.
Boti iliripotiwa kupoteza muelekeo ilikuwa inatokea Senegal mwezi mmoja uliopita ikiwa na watu takriban 100.
Inaaminika kuwa boti hiyo ilikuwa inaelekea katika visiwa vya Canary vya Uhispania, kituo maarufu kwa wahamiaji wanaokwenda Umoja wa Ulaya.
Maelfu ya watu wanakimbia umaskini na vita na kuhatarisha maisha yao kwa kufanya safari hatari kila mwaka.
Watu hawa wanafanya safari mara nyingi katika boti za kawaida au majahazi ambayo hutumiwa na wanaofanya biashara ya magendo.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.