Wahamiaji 41 wafariki katika ajali ya meli kwenye Bahari ya Mediterranian

Walinzi wa pwani ya Italia wakiwasaidia wahamiaji kuingia katika boti baada ya kuwaokoa wahamiaji katika operesheni maalum kusini mwa Lampedusa, Picha ilitolewa Aug. 6, 2023, (Picha na Italian Coastguard / Guardia Costiera / AFP)

Wahamiaji 41 wamekufa katika ajali ya meli wiki iliyopita katikati mwa bahari ya Mediteranian , shirika la habari la Ansa limeripoti leo likinukuu watu walionusurika ambao waliwasili muda baadaye kwenye  kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

Ansa limesema watu wanne walionusurika katika ajali hiyo wamewaambia waokoaji kwamba walikuwa katika boti iliyokuwa imebeba watu 45 wakiwemo watoto watatu.

Boti hiyo iliondoka Alhamisi asubuhi kutoka Sfax, nchini Tunisia ambako ndiyo kitovu cha mzozo wa wahamiaji lakini ilizama saa chache baadaye, walionusurika walikaririwa wakisema.

Walionusurika ni wanaume watatu na mwanamke mmoja kutoka Ivory coast na Guinea wamesema waliokolewa na meli ya mizigo na baadae kuhamishiwa katika meli ya ulinzi wa ufukweni ya italia. Haikuthibitishwa kama taarifa zilizotolewa na Ansa lilihusisha boti mbili zilizopata ajali ambazo walinzi wa ufukwe walitoa taarifa zake jumapili , wakisema kuwa watu 30 walikuwemo ndani lakini hawajulikani walipo.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.