Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:33

Ugiriki inataka kutumia fursa ya mazingira mazuri ya kisiasa na jirani yake Uturuki


Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis akiwa Athens. Oct. 27, 2022.
Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis akiwa Athens. Oct. 27, 2022.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amesema hiyo haimaanishi kuwa Uturuki imebadili msimamo wake juu ya tofauti kuu kati ya nchi hizo mbili na inahitaji kuachana na tabia yake ya uchokozi na kinyume cha sheria dhidi ya uhuru wa Ugiriki na uadilifu wa eneo

Waziri Mkuu wa Ugiriki amesema Jumatatu serikali yake inataka kutumia kikamilifu fursa ya mazingira mazuri ya kisiasa na nchi jirani ya Uturuki kuboresha uhusiano wa nchi hizo mbili licha ya kuwepo kwa mzozo wa miongo kadhaa.

Lakini Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amesema hiyo haimaanishi kuwa Uturuki imebadili msimamo wake juu ya tofauti kuu kati ya nchi hizo mbili na inahitaji kuachana na tabia yake ya uchokozi na kinyume cha sheria dhidi ya uhuru wa Ugiriki na uadilifu wa eneo.

Uturuki na Ugiriki bado zinatofautiana kuhusu mipaka ya baharini katika eneo la mashariki mwa Mediterrania, mzozo ambao unaathiri uingiaji usio wa kawaida wa wahamiaji katika Umoja wa Ulaya, haki za madini na makadirio ya nguvu za kijeshi.

Mitsotakis alisema alikubaliana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mkutano wa NATO huko Vilnius, Lithuania hapo Julai 11 hadi 12 kuanzisha njia mpya ya mawasiliano na kudumisha kipindi cha utulivu.

Forum

XS
SM
MD
LG