Wafaransa wajiandaa na uchaguzi wenye ushindani mkali

Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal (kulia) akila ice cream wakati alipokuwa katika kampeni ya kuwaunga mkono wabunge wanaomaliza muda wao na wagombea wa chama tawala huko Lyon June 28, 2024. Picha na LIVIER CHASSIGNOLE / AFP

Wafaransa wanajitayarisha kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge siku ya jumapili ambao huwenda matokeo yakasababisha serikali ya Rais Emmanuel Macorn kupoteza wingi wa viti vyake bungeni na kukipata ushindi kwa mara ya kwanza chama chenye siasa kali za kulia.

Ukusanyaji wa maoni unaonesha kwamba wafaransa wanachukulia kwa dhati uchaguzi huu kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka 25, katika kuamua ikiwa wa wakabidhi chama cha Rally National RN cha siasa kali za kulia jukumu la kupanga sera za ndani ya nchi yao.

Chama hicho cha Marine le Pen kinaongoza kwenye maoni kikitarajiwa kupata kati ya asili mia 33 hadi 36 kikifuatwa na mungano wa vyama vya mrengo wa kushoto na mungano wa siasa za kati unaongozwa na rais Emmanuel Macron kushika nafasi ya tatu.

Lakini kutokana n a mfumo wa duru mbili za uchaguzi ni vigumu kutabiri jinisi matokeo yatakavyoweza kutokea. Duruy a pili itafanyika hapo Julai 7.