Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:06

Vyama vya siasa vya mrengo wa kulia vimepata mafanikio makubwa Ulaya


Vyama vya siasa vya mrengo wa kulia vimepata mafanikio makubwa katika uchaguzi wa wabunge wa Umoja wa Ulaya Jumapili, vikikabiliana na kushindwa kwa viongozi wawili muhimu wa umoja huo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz.

Nchini Ufaransa, chama cha National Rally cha Marine Le Pen kimetawala uchaguzi huo kiasi kwamba kimemfanya Rais Macron, kuvunja bunge la taifa mara moja na kuitisha uchaguzi mpya.

Ilikuwa bahati nasibu kubwa ya kisiasa kutokana na chama kuwa katika hatari ya kupoteza zaidi, na kushikilia muhula wake wote wa urais ambao unamalizika 2027.

Le Pen alifurahi kukubali changamoto hiyo.

“Tuko tayari kugeuza hali ya nchi, tupo tayari kutetea masilahi ya Wafaransa na kukomesha wimbi la wahamiaji,” amesema, akirudia ujumbe wa viongozi wengi wa mrengo wa kulia kutoka nchi zingine ambao walikuwa wakisherehekea huo.

Forum

XS
SM
MD
LG