Idadi hiyo inaongeza kwenye maelfu ya ajira ambazo zimepangwa kuondolewa kwenye sekta ya uchimbaji madini kutokana na changamoto za miundombinu, pamoja na kushuka kwa bei za bidhaa. Kumba ambayo ni sehemu ya kampuni ya Anglo American, Desemba ilisema kuwa itapunguza uzalishaji, ili kuendana na uwezo mdogo wa shirika la reli la Transnet.
Shirika hilo linalomilikiwa na serikali katika miaka ya karibuni limekabiliwa na uhaba wa mabehewa na vipuri, pamoja na wizi wa nyaya na reli. Kupitia mkutano wa kimitandao mapema , mkurugenzi mkuu wa Kumba, Mpumi Zikalala amesema kwamba kupunguzwa kwa nafasi za ajira, pamoja na marekebisho kwenye utawala wa ofisi kuu yalioanza Septemba mwaka jana, kutaathiri asilimia 10 ya wafanyakazi wake.
Ameongeza kusema kwamba hatua hizo ni muhimu ili kuhakikisha kampuni inabaki kwenye hali ya ushindani.