Kesi hiyo inafuatia ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari unaofanywa na utawala wa kijeshi kwa miezi kadhaa nchini kote ambako radio nne binafsi na vituo viwili vya televisheni binafsi vilipigwa marufuku mwezi Mei.
Katika maoni yao kwa waandishi wa habari tarehe 12 Juni, Djene Diaby na Tawel Camara, wawili kati ya makamishna 13 wa mdhibiti wa vyombo vya habari HAC, waliwatuhumu wamiliki wa vyombo vya habari ambavyo sasa vimepigwa marufuku, kupokea hongo kutoka kwa serikali ya kijeshi kama malipo ya utangazaji unaopendelea serikali hiyo.
Hata hivyo, vyombo hivyo vya habari viliendelea kuokosoa utawala wa kijeshi ambao ulivipiga marufuku mwezi uliopita, makamishna hao walidai.
Diaby na Camara walishtakiwa kwa kumkashifu rais na kuzuiliwa katika gereza kuu la mjini Conakry, mwenzano Amadou Toure aliiambia AFP.
Makamshina hao wawili walifika mahakamani mjini Conakry Jumatano, ambako waliomba msamaha na kusema hawakuwa na ushahidi wa madai yao.
Kesi yao imeahirishwa hadi leo Alhamisi.