Makundi ya kimataifa ya haki za binadamu na Umoja wa Mataifa waliwaomba wabunge kutupilia mbali mswada huo, wakisema unatishia mafanikio ya miaka kadhaa na ungeifanya Gambia kuwa nchi ya kwanza kubatilisha mafuruku ya ukeketaji wa wanawake.
Wabunge walitupilia mbali rasimu ya sheria hiyo kwa kupiga kura dhidi ya vifungu vyake vyote vilivyopendekezwa.
“Mswada wa marekebisho ya sheria ya Wanawake ya mwaka 2024, baada ya kupitia hatua ya kuzingatiwa na vifungu vyote kupigiwa kura, umekataliwa,” alisema Fabakary Tombong Jatta, Spika wa Bunge la Gambia, akiongeza kuwa mchakato wa kutunga sheria “umekwisha”.
Wanaharakati wanaopinga ukeketaji walicheza na kuimba nje ya bunge baada ya mswada huo kukataliwa, mwanaharakati Absa Samba aliiambia AFP kwa njia ya simu.