Wabunge nchini Gabon walikutana Alhamisi kuanza kujadili rasimu ya katibu mpya, hatua ya kwanza kuelekea kurejeshwa kwa serikali ya kiraia, ambayo utawala wa kijeshi uliahidi kufuatia mapinduzi ya 2023.
Mapinduzi hayo yalihitimisha utawala wa miaka 55 wa familia ya rais wa zamani Ali Bongo Ondimba, na katiba hiyo mpya itapendekeza kufuta wadhifa wa waziri mkuu na muhula wa urais wa miaka saba, unaoweza kuongezwa mara moja.
Wagombea wa urais wanapaswa kuwa watoto wa wazazi waliozaliwa nchini Gabon kulingana na rasimu hiyo iliyopendekezwa inayoonekana kusambazwa mtandaoni.
Rasimu hiyo ya katiba mpya inafafanua pia kwamba ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke na italazimisha kuhudumu katika jeshi ikihitajika, huku ikithibitisha Kifaransa kama lugha rasmi ya nchi.