Waasi hao wanaoongozwa na Watuareg walisema waliua wapiganaji 84 wa Wagner na wanajeshi wa Mali 47 katika siku tatu za mapigano makali ambayo yalianza tarehe 25 Julai kwenye kambi ya kijeshi katika mji wa Tinzaouatene.
Muungano wa waasi hao, Strategic Framework for the Defence of the People of Azawad ( CSP-DPA) ulisema wanajeshi wengine 30 au wapiganaji, aidha “walikufa au walijeruhiwa vibaya” na kusafirishwa kwa ndege katika mji wa kaskazini wa Kidal.
Azawad ni jina la jumla kwa maneno yote ya Tuareg Berber, hasa katika sehemu kubwa ya kaskazini mwa Mali na magharibi mwa Niger. Waasi hao wanaotaka kujitenga wanapigania kuwa na nchi yao.
Muungano huo wa waasi ulisema waliwateka nyara wapiganaji saba wa Wagner na serikali ya Mali na kusema walipoteza wapiganaji wao tisa katika mapigano.
AFP haikuweza kuthibitisha idadi hiyo ya vifo kutoka kwa vyanzo huru. Jeshi la Mali na Kundi la Wagner walikiri kupata hasara kubwa katika eneo hilo.